Dk. Yonazi ampongeza Balozi Mutatembwa

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dk. Jim Yonazi amempongeza Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Anderson Mutatembwa kwa Kuteuliwa kuwa Balozi.

Dk. Yonazi ametoa pongezi hizo Tarehe 16 Desemba 2024, wakati akimuaga Balozi Mutatembwa na kumakaribisha Naibu katibu Mkuu mpya Dk. James Kilabuko.

Dkt. Yonazi amempongeza Balozi Mutatembwa kwa kufanya kazi ya ushauri kwa utulivu aliyotokana hekima aliyojijengea na kujaliwaa na Mwenyezi Mungu kuwa nayo “Na ndiyo maana Mhe. Rais ameweza kukuamini na kukuteuwa katika nafasi ya Ubalozi ili uweze kumuwakilisha yeye pamoja na Nchi katika maeneo ambayo atakayoona inampendeza.” Alifafanua

Aliendelea kusema kuwa, nafasi ya ubalozi ni nafasi nyeti na adhimu sana na ni fursa inayopatikana kwa watu wachache sana, “umepata fursa nyeti sana ya kuitumikia Taifa naamini utaendelea kufanya kazi kama ambavyo umekuwa ukifanya hapa na utakaoenda kufanya nao kazi watafaidika na kufurahia kama tulivyo faidika sisi.” Alibainisha Dk. Yonazi

Akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya Dk. James Kilabuko, Katibu Mkuu Dk. Yonazi alisema Ofisi ya Waziri Mkuu ni Ofisi yenye majukumu mazito yenye watumishi wachapakazi wenye kutizama tija katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Naibu Katibu Mkuu, Dk. James Kilabuko Alimshukuru Rais kwa kumteuwa katika nafasi hiyo na kuona kwamba anaweza kumsaidia Katibu Mkuu Kiongozi katika nafasi hiyo, aliendea kusema kuwa anategemea kupata ushirikiano kutoka kwa Watumishi na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika kumsaidia Katibu Mkuu Dk. Jonazi kiutendaji na kufikia malengo yanayotegemewa na mamlaka za juu.

Kwa Upande wake Balozi Anderson Mutatembwa , alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea Kumuamini na kumteuwa katika nafasi hiyo.

Aidha, Ameishukuru Menejimenet ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano waliomupatia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ofisini hapo, aliendelea kusema kuwa ni sehemu ambayo atapakumbuka kwani amefanya kazi kwa amani na Utulivu wa hali ya juu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *