Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeBiasharaDkt Samia aanika mikakati Tanzania kujitegemea kwa ngano

Dkt Samia aanika mikakati Tanzania kujitegemea kwa ngano

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itaangalia upya mikataba na wawekezaji walioshindwa kuyaendeleza mashamba ya ngano wilayani Hanang mkoani Manyara, ili yagawiwe kwa wakulima wazalishe ngano.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, mkakati wa Serikali yake ni kuufanya Mkoa wa Manyara uzalishe ngano kukidhi mahitaji ya nchi na kuondoa utegemezi wa zao hilo kutoka mataifa mengine duniani.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa, Oktoba 3, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais, uliofanyika wilayani Hanang katika Mkoa wa Manyara.

Amesema kwa mikakati hiyo, analenga kufikia mwaka 2030, Mkoa wa Manyara uzalishe tani milioni moja ya zao hilo na kuondoa uagizaji wa ngano kutoka nje ya nchi.

“Ili tuweze kujitegemea kwa mahitaji ya ngano. Kilimo kikubwa huku ni ngano, kwa hiyo tunataka Hanang ituzalishie ngano tani milioni moja ifikapo mwaka 2030,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, Serikali itaangalia upya mikataba na wawekezaji wenye mashamba makubwa na wakashindwa kuyaendeleza ili yagawiwe kwa wakulima kwa ajili ya uzalishaji wa ngano.

“Haipendezi tuna mashamba yanayoweza kuzalisha ngano nyingi, lakini tunaagiza ngano nyingi kutoka nje nah uku mashamba yamekaa hayazalishi, kwa hiyo tunakwenda kuyaangalia mashamba hayo,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments