Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia aeleza anavyofarijika kutimiza ndoto ya Msuya

Dkt Samia aeleza anavyofarijika kutimiza ndoto ya Msuya

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema miongoni mwa faraja alizonazo katika uongozi wake, ni kutimiza ndoto ya Waziri Mkuu mstaafu, hayati Cleopa Msuya ya kukamilisha mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Septemba 30, 2025 katika Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, alipokuwa katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, mradi huo na ule wa Barabara ya Msuya ni miongoni mwa miradi ambayo hayati Msuya alimfuata na kumwona aitekeleze.

“Faraja yangu ni kwamba nimeweza kutimiza mradi ambao, marehemu Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya ulikuwa ni mradi wake wa kufa na kupona.

“Alinifuata na kuniomba miradi mikubwa miwili mradi mmoja maji, Same-Mwanga-Korogwe na mradi wa pili ni barabara ile Msuya Bypass Faraja yangu ni kwamba miradi yote miwili nimeweza kuifanya ameiona kabla Mungu hajamchukua,” amesema.

Hadi sasa, amesema tayari awamu ya kwanza ya mradi huo, imekamilika na wananchi wa Mwanga wameanza kupata huduma, huku awamu ya pili ikitarajiwa kuwanufaisha wananchi wa Same na Korogwe.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments