Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeBiasharaDkt Samia: Kipaumbele changu wachimbaji madini wadogo

Dkt Samia: Kipaumbele changu wachimbaji madini wadogo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema wachimbaji wadogo wa madini bado kipaumbele chake, akiahidi kwenda kumaliza migogoro inayowakabili baina yao wenye migodi mikubwa.

Dk. Samia ametoa ahadi hiyo, leo Jumamosi Oktoba 11, 2025 akihutubia mkutano wa hadhara Maganzo Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni mkutano wake wa kwanza wa mkoani hapa, akitokea Simiyu.

“Niwashukuru wachimbaji wadogo kwa sababu wamesaidia sana kuongeza mapato kwenye sekta ya madini. Asilimia 40 ya mapato tunayoyapata yanatokana na wachimbaji wadogo, hivyo wachimbaji wadogo bado kipaumbele chetu,”

“Natambua kulikuwa na migogoro baina ya mgodi mkubwa, wadogo na wananchi, tumeanza kuishughulikia mkitupa ridhaa tunakwenda kuimaliza na haitakuwepo. Ndugu zangu wachimbaji niwaahidi bado tunakwenda kuifanya kazi yenu,” amesema Dk.Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments