Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Nataka matokeo kwa wananchi sio michakato inaendelea

Dkt Samia: Nataka matokeo kwa wananchi sio michakato inaendelea

Rais Dk Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri na naibu mawaziri wake, huku akiwaeleza katika muhula wa pili wa Serikali yake, anataka kuona matokeo kwa wananchi sio ofisini.

Amewaambia mawaziri hao kuwa, katika utendaji wao hatapenda kusikia neno kuwa ‘tunaendelea’ au ‘mchakato upo mbioni’ bali matokeo pekee kwa wananchi.

Mkuu huyo wa nchi, ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Novemba 18, 2025 alipozungumza wakati wa hotuba yake ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Tukikubaliana mradi ni matokeo kwa wananchi si ofisini kwako, tumefikia hapa, bado hapa hapana…matokeo kwa wananchi kwa muda tutakaokubaliana,” amesema Dk Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments