Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeAfyaDkt. Samia: Nitaendelea kuboresha huduma za afya

Dkt. Samia: Nitaendelea kuboresha huduma za afya

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kujenga hospitali, zahanati na vituo vya afya vyenye vifaa kamili vya matibabu ili kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Akihutubia mkutano wa hadhara leo Jumanne, Septemba 30, 2025, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Dkt. Samia alisema ujenzi huo utashirikiana na upatikanaji wa dawa za uhakika na watumishi wa afya wenye uwezo.

Dk. Samia alikumbuka changamoto alizokutana nazo mwaka 2015 alipokuwa mgombea mwenza, wakati akifika Hedaru wilaya Same kuomba kura. Alisema alishangazwa na hali mbaya ya zahanati, ambazo hazikuwa na vifaa vya kutosha, huku watoa huduma wakiendelea kuhudumia wanawake wajawazito.

“Pale nilikuta kizahanati kibovu sana, kilichonisikitisha walikuwa wanatoa huduma za kina mama kujifungua. Lakini hali nilioiona haikunifurahisha hata kidogo. Pamoja nilikuwa mgombea mwenza, ila niliweka nia ya kurekebisha hali ile Tanzania nzima. Leo nashukuru Mungu nimeweza kuirekebisha, nimeweza sana…na tutaendelea kujenga hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati zenye zana kamili,” alisema Dk. Samia.

Dk. Samia aliongeza kuwa malengo ya serikali ni kuhakikisha vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua vinapungua, kwa hivyo ahadi yake ya kuendeleza ujenzi na kuboresha huduma za afya ni sehemu ya mkakati huo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments