Saturday, October 11, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Nitajenga skimu za umwagiliaji 738, kukuza kilimo

Dkt Samia: Nitajenga skimu za umwagiliaji 738, kukuza kilimo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi ujenzi wa skimu 738 za umwagiliaji ili kuboresha na kukuza sekta ya kilimo nchini.

Dk. Samia amesema kwa sasa kwenye sekta ya kilimo kipaumbele ni kilimo cha umwagiliaji maji na skimu hizo zitajengwa kote nchini.

Ametoa ahadi hiyo, leo Jumamosi Oktoba 11, 2025 akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Maswa mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya kuwaaga wananchi wa mkoa huo, baada ya kuihitimisha ziara ya kampeni zake na kuhamia Mkoa wa Shinyanga.

“Kilimo cha umwagiliaji maji ndicho kipaumbele chetu, tunakwenda kujenga skimu za umwagiliaji 738 Tanzania nzima, hadi mwaka huu. Lengo ni kukuza sekta ya kilimo ifikapo 2030, nikitoka kwenda kupumzika niache sekta ya kilimo imekuwa kwa asilimia 10 kwa mwaka,”

“Sasa hivi tunakuwa kwa asilimia 4 hadi tano, nataka niikuze kwa asilimia 10 kwa mwaka ili ndilo lengo langu. Ninapozungumza sekta ya kilimo ni mifugo na uvuvi vyote vinaingia kwenye kilimo,” ameeleza.

Dk. Samia amefichua kuwa mkakati wa Serikali yake ni kukuza biashara na viwanda, ili kutoa ajira wa vijana wanaomaliza vyuo vya ufundi vya Veta.

Mbali na hilo, Dk Samia ameaahidi ujenzi wa barabara ndani ya mkoa wa Simiyu ili kuunganisha makao makuu za wilaya na mkoa huo, sambamba na kuziunganisha kata na makao makuu za wilaya.

Pia, Dk Samia amesema Maswa kutakuwa na kituo kikubwa cha reli ya kisasa ya SGR inayotokana Tanga-Arusha hadi Musoma, ambapo abiria watashuka na kupanda.

“Kituo kitakuwa na fursa za biashara na kuongeza fursa za ajira kwa vijana wetu hawa,” amesema Dk Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments