Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Nitajenga soko, barabara za kutosha Arusha

Dkt Samia: Nitajenga soko, barabara za kutosha Arusha

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake inatarajia kujenga soko kubwa la machinga na kukamilisha soko la kisasa la wafanyabiashara katika eneo la Bondeni City mkoani Arusha.

Sambamba na masoko hayo, ameahidi kujenga barabara katika kila wilaya mkoani humo, ikiwemo ya Malula-Ngarenanyuko iliyotengewa Sh30 bilioni na Tengeru-Mbuguni-Mirerani yenye urefu wa kilomita 24 wilayani Monduli.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Oktoba 2, 2025 alipozungumza na wananchi wa Arusha Mjini, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema ujenzi wa soko hilo la kisasa, utaambatana na ujenzi wa soko la machinga katika eneo la Bondeni City mkoani humo, kurahisisha biashara.

Ameahidi kukamilika miradi inayoendelea na kutekeleza mipya iliyoorodheshwa katika ilani ikiwemo Barabara ya Malula-Ngarenanyuko iliyotengezwa Sh30 bilioni na Tengeru-Mbuguni-Mirerani yenye urefu wa kilomita 24 na upembuzi yakinifu umeshafanyika.

Amesema Monduli itajengwa Barabara ya Mto wa Mbu-Serera na mkataba unatarajiwa kusainiwa na upembuzi yakinifu umefanyika katika kipande cha Sarera-Engaruka kilomita 27 na anatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Amesema Barabara ya Engaruka-Ngaresero yenye urefu wa kilomita 24, zabuni inatarajiwa kutangazwa, huku wilayani Karatu akitarajia kutekeleza mradi wa Barabara ya Mahotelini yenye urefu wa kilomita 10.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments