Dodoma Jiji imeachana na kiungo Ibrahim Ajib kutokana na utovu wa nidhamu, licha ya kuonywa mara kadhaa.

Msemaji Moses Mpungu amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwa mfano kwa wachezaji wengine. Ajib, aliyewahi kuchezea Simba na Yanga, alisimamishwa mwishoni mwa msimu uliopita kwa kosa hilo.
Dodoma Jiji imekamilisha kwa asilimia 90 usajili wake, ikiwemo kuongeza mikataba ya wachezaji wake nyota na kusajili wachezaji wapya watatu, lengo likiwa kumaliza ligi kwenye nafasi za juu.


