Tuesday, February 10, 2026
spot_img
HomeHabariEWURA yatoa msaada mashuka 455 Hospitali ya Mkoa Iringa

EWURA yatoa msaada mashuka 455 Hospitali ya Mkoa Iringa

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo, 10 Februari 2026, imetoa msaada wa mashuka 455 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma za kimatibabu hospitalini hapo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio la Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, lililofanyika mkoani humo tarehe 9 hadi 10 Februari 2026. 

 Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Nuru Siyovelwa, amepokea msaada huo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa, na kueleza kuwa, mashuka yamekuwa hayatoshelezi katika hospitali za mkoa huo, hivyo ameishukuru EWURA kwa kuguswa kwani yatasaidia kutoa huduma bora kwa wananchi.

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Alfred Mwakalebela, ameeleza kuwa mashuka hayo yatapunguza  changamoto iliyokuwepo ya upungufu wa mashuka, kwani kwa siku, kila mgonjwa anatakiwa kutumia mashuka 6, ilhali kwa sasa  huduma hiyo haitoshelezi kwa kila mgonjwa. 

Akiwasilisha msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Mha. Hawa Lweno, amesema kuwa EWURA itaendelea na utaratibu wa kutoa mchango kwa jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo afya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments