Saturday, March 14, 2026
spot_img
HomeHabariEWURA yatua Singida, Iringa kuhamasisha nishati safi ya kupikia

EWURA yatua Singida, Iringa kuhamasisha nishati safi ya kupikia

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  Kanda ya Kati, imeendelea kutoa hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Singida na Iringa sanjari na kuvutia uwekezaji wa bidhaa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia.

Hamasa hiyo imetolewa  na Meneja wa EWURA, Kanda ya Kati, Mha. Hawa Lweno, kupitia vipindi vya redio mkoani Singida na Iringa pamoja na semina  kwa mama lishe, waendesha bodaboda na wasambazaji wa gesi ya kupikia (LPG), iliyofanyika kati 27 na 29 Mei, 2025. 

“ Lengo letu ni kuhakikisha watumiaji wa gesi ya kupikia wanazingatia masuala ya usalama, afya na utunzaji wa mazingira pamoja na kuhakikisha watoa huduma tunaowadhibiti wanafuata na kutii masharti ya leseni zao” amesisitiza Mha. Lweno.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments