Fadlu Afunguka, aitaja Dabi

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amethibitisha rasmi kuwa timu yake inajiandaa kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga utakaopigwa Juni 25, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Fadlu alitoa kauli hiyo baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Kengold FC, akieleza kuwa kwanza watakamilisha mchezo dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kuelekeza nguvu zote kwenye dabi.

Amezima tetesi za Simba kutoshiriki mechi hiyo, akisema: “Baada ya Kagera Sugar, tunaanza maandalizi ya dabi dhidi ya Yanga.”

Katika ushindi huo dhidi ya Kengold, Kibu Denis alipachika mabao mawili na kufikisha manne msimu huu, akisema Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi umekuwa na bahati kwake na kwa timu. Mabao mengine yalifungwa na Elie Mpanzu, Leonel Ateba na Jean Ahoua (16 kwa msimu).

Kocha wa Kengold, Omari Kapilima, alikiri ubora wa Simba na kueleza kuwa wameanza maandalizi ya Ligi ya Championship baada ya kushuka daraja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *