Thursday, March 12, 2026
spot_img
HomeMichezoFadlu kuwatumia Ahoua na Maema Ngao ya Jamii

Fadlu kuwatumia Ahoua na Maema Ngao ya Jamii

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amesema anapanga kuwatumia viungo washambuliaji Jean Charles Ahoua na Neo Maema kwa pamoja kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Septemba 16, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Fadlu alisema anataka kuongeza ubunifu eneo la ushambuliaji ili kuwarahisishia kazi mastraika Selemani Mwalimu na Steven Mukwala, akibainisha kuwa ubora na ushirikiano wa wachezaji hao unaweza kuvunja ngome ya wapinzani.

Hata hivyo, Simba itaikosa huduma ya Jonathan Sowah kutokana na kadi nyekundu aliyopata akiwa Singida Black Stars kwenye fainali ya Kombe la FA.

Wakati huo huo, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Simba Day, Septemba 10, ambapo kikosi kipya kitapewa rasmi kwa mashabiki, huku baadhi ya wachezaji wapya akiwemo beki chipukizi Vedastus Masinde wakitarajiwa kutambulishwa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments