Fountain Gate kutangaza kocha mpya

Fountain Gate imesema muda wowote itamtambulisha Kocha Mkuu mpya wa kimataifa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Issa Liponda alisema kikosi kipo kambini Morogoro kikiendelea na mazoezi na pia wanatafuta mechi za kirafiki ili kuongeza viwango vya wachezaji.

Aliongeza kuwa wamesajili wachezaji wenye ubora wa kimataifa kuhakikisha msimu ujao wanashika nafasi za juu, huku akiwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *