Fountain Gate yaweka kambi Morogoro, yafuta saba

Fountain Gate imetangaza kambi ya maandalizi ya msimu mpya kufanyika Morogoro. Klabu hiyo ilinusurika kushuka daraja baada ya kushinda mechi ya mchujo dhidi ya Stand United kwa jumla ya mabao 5-2.

Klabu hiyo yenye makazi yake Babati, Manyara, pia imeachana na wachezaji saba, akiwemo kiungo nyota Salum Kihimbwa, ambaye tayari amejiunga na Mashujaa FC. Wengine walioachwa ni Kelvin Nyanguge, Paul Ulomi, Joram Mgeveke, Shafik Batambuze, Amosi Kadikilo na Said Mbatty.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *