Hatua ya Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwa kinara wa nishati safi, imetajwa kufungua milango ya uwekezaji wa teknolojia katika sekta hiyo, ikiwemo kuanza kutumika kwa magari ya nishati ya umeme yatakayopunguza athari za mazingira nchini.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, Dkt Samia amekuwa na msimamo na maono makubwa katika sekta hiyo na mwaka 2022 alizindua mkakati wa matumizi ya nishati safi nchini.
Mhandisi Mramba ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Machi 6, 2026 alipozungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Zera inayoingiza na kutengeneza magari hayo ya umeme nchini.
“Tangu hapo ameendelea kuwa kinara wa matumizi ya nishati safi sio kwa kupikia tu, lakini hata kwa matumizi mengine yakiwemo haya ya vyombo vya usafiri,” amesema Mramba.




