Kocha wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi, amesema ameona mwanga wa mafanikio ya timu yake baada ya michezo ya Kagame Cup.
Akizungumzia maendeleo ya kikosi chake, Gamondi alisema anajivunia usajili na nidhamu ya wachezaji wake, huku akiona nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.
Kocha huyo alisema Kagame Cup imewasaidia kujua mapungufu na kuimarisha kikosi chenye ushindani zaidi.
Singida Black Stars imefuzu nusu fainali ya mashindano hayo ikiwa na pointi saba.




