Sunday, April 5, 2026
spot_img
HomeMichezoHakimi aizungumza AFCON 2025: “Tulingoja sana, ushindi ni ushindi!”

Hakimi aizungumza AFCON 2025: “Tulingoja sana, ushindi ni ushindi!”

Kapteni wa timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi, ameonesha furaha yake baada ya Atlas Lions kutwaa ubingwa wa AFCON 2025, mafanikio yaliyokuja kufuatia uamuzi wa CAF kuiondolea Senegal taji hilo na kulikabidhi kwa Morocco.

Hakimi alitoa kauli hiyo alipokuwa mgeni kwenye podcast The Bridge pamoja na nyota wenzake Kylian Mbappé na Aurélien Tchouaméni, ambapo alikiri kuwa alikuwa akisubiri kwa muda mrefu kuona taifa lake likifikia mafanikio hayo makubwa.

“Kwa namna yoyote ile tulivyopaswa kulichukua kombe hili, sisi tunalichukua. Tunafurahi sana. Niliisubiri kwa muda mrefu moment hii. Hata kama ushindi ulikuja kwa njia hii, tumeshinda,” amesema Hakimi.

Kama nahodha aliyeiongoza Morocco kwenye mashindano hayo, Hakimi amesema taji hilo lina maana kubwa sana kwake binafsi na kwa taifa zima, hasa ukizingatia safari ndefu ya timu hiyo na presha ya kucheza mbele ya mashabiki wao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments