Hope Holdings yashirikiana na Bolt Business kidijitali usambazaji wa mazulia

Hope Holdings, kampuni ya uwekezaji wa ndani ambayo iliajiri zaidi ya wafanyakazi 450 ndani ya Tanzania mwaka 2024, imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Bolt Tanzania kwa ajili ya kudijitali shughuli za biashara ya mazulia kupitia chapa yake ya Amal Carpets, kwa kutumia mtandao mpana wa huduma za usafirishaji wa Bolt kufikisha bidhaa moja kwa moja kwa wateja.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, hatua hii ni sehemu muhimu ya mkakati wao wa kufikisha bidhaa majumbani bila kuacha familia moja. Hili ni kwa njia mpya na yakidigitali, ikiwa ni juhudi ya kupambana na mitazamo hasi ya chapa inayochochewa na wauzaji wa kati wanaouza mazulia kwa bei za juu zisizodhibitiwa.

“Tunataka kuondoa dhana kwamba mazulia ya Amal ni ya bei ghali na si kwa ajili ya watu wa kawaida,” alisema Micky Decha, meneja wa masoko wa Amal Carpets.
 “Kupitia suluhisho la kidijitali, tunaweza kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuwapa bidhaa bora kwa bei nafuu na zinazodhibitiwa,” aliongeza.

Kwa kutumia huduma ya Bolt Business, wateja sasa wataweza kuagiza mazulia moja kwa moja na kuyapokea nyumbani, hali itakayosaidia kuondoa urasimu wa maonyesho ya bidhaa, ucheleweshaji wa usafirishaji, na gharama za wauzaji wa kati.

“Ushirikiano huu unalenga kufikiria upya jinsi biashara za Kitanzania zinavyoweza kudijitali baadhi ya shughuli zao ili kuwafikia wateja wa kipato cha chini kwa bidhaa zenye ubora,” alisema Milu Kipimo, Meneja wa Bolt Business kwa nchi za Tanzania, Kenya na Tunisia.

Kwa upande wa Hope Holdings — ambayo pia inamiliki chapa maarufu kama LC Waikiki na Papparotti — huu ni mpango wake wa kwanza wa kidijitali unaomlenga moja kwa moja mlaji wa kawaida. Kampuni hiyo inasema huu ni mwanzo tu wa mikakati mipana ya kudijitalisha mifumo yake ya usambazaji, kwa lengo la kuhakikisha bei shindani na kuongeza thamani zaidi kwa wateja wengi kwa wakati mmoja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *