Beki wa kati wa Simba, Hussein Kazi, amejiunga na Namungo FC kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na Simba.

Kiongozi wa Namungo amethibitisha usajili huo, akisema walipambana kumnasa kutokana na timu nyingi kumtaka.
Kazi alijiunga na Simba mwaka 2023 kutoka Geita Gold lakini hakupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Namungo pia inadaiwa kummezea mate kipa wa Simba, Ally Salim, kama mbadala wa Beno Kakolanya kwa msimu ujao.