Ibenge afichua sababu Azam kufungwa na JKT Tanzania

Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema uchovu wa mazoezi magumu na kukosekana kwa wachezaji 12 walioko kwenye michuano ya CHAN 2024 ndizo sababu za kupoteza 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mechi ya kirafiki jijini Arusha.

Ibenge amesema mchezo huo ulikuwa kipimo cha kuangalia mapungufu na mifumo ya timu kabla ya mashindano ya kimataifa.

Mabao ya JKT yalifungwa na Laurian Makame na Najim Magulu, huku Azam ikipata bao kupitia Yoro Diaby.

Kocha wa JKT, Ahmad Ally, aliwasifu vijana wake kwa kiwango kizuri licha ya kuandaliwa kwa siku nane tu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *