Monday, February 16, 2026
spot_img
HomeBiasharaInfinity Developments yazindua mradi wa kimkakati wa makazi wa dola milioni 250...

Infinity Developments yazindua mradi wa kimkakati wa makazi wa dola milioni 250 Zanzibar

Zanzibar, Februari 16. Kampuni ya Infinity Developments imezindua rasmi mradi wa makazi na matumizi mchanganyiko wa Infinity Hills katika eneo la Kikwajuni, Stone Town, baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria.

Infinity Hills unatarajiwa kuwa na makazi ya kisasa yatakayoweka viwango vipya vya maisha ya mjini Zanzibar, kwa kuunganisha urahisi wa huduma za mijini na uzuri wa asili wa kisiwa hicho.

Mradi huo utajumuisha jumla ya nyumba 1,112 zilizobuniwa kisasa, zikiwemo studio, nyumba ya vyumba viwili vya kulala na nyumba ya chumba kimoja cha kulala, pamoja na maeneo ya biashara na ofisi.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Mwenyekiti wa Infinity Developments, Samuel Saba, alisema Infinity Hills ni kielelezo cha dhamira ya muda mrefu ya kampuni hiyo katika kujenga makazi ya kisasa, yenye ubora wa hali ya juu na yanayoendana na mahitaji ya baadaye Zanzibar.

“Nina furaha kubwa kutambulisha Infinity Hills, mradi wa makazi wenye maono mapana uliobuniwa kuleta muunganiko kamili wa faraja, urahisi na ustaarabu wa kisasa,” alisema Bw. Saba.

“Mradi huu uko katika eneo la kimkakati  ukiendana na upekee wa Zanzibar huku ukitoa mtindo wa maisha wa kisasa na wa hadhi ya juu,” aliongeza kusema.

Mradi huo umejengwa jirani na bustani ya umma iliyopambwa kwa mandhari nzuri na upo karibu na ufukweni. Infinity Hills unaunganisha makazi na maeneo ya wazi ya kijani, migahawa na huduma za burudani. Aidha, uko dakika chache kutoka Stone Town na karibu na miundombinu muhimu ya kijamii, ikiwemo GEMS Zanzibar International School pamoja na vituo muhimu vya afya.

“Infinity Hills si tu mahali pa kuishi; ni jamii inayojenga hisia halisi ya kuwa sehemu ya pamoja,” aliongeza Bw. Saba.

“Kuanzia migahawa ya kuvutia na mabwawa ya kuogelea hadi maeneo yaliyobuniwa kwa ajili ya mapumziko na mwingiliano wa kijamii, kila kipengele kinaakisi dhamira yetu ya ubora, ubunifu na thamani ya muda mrefu,” alisema.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, mradi huo utakuwa na bwawa la kuogelea la pamoja, bustani zilizopangwa kitaalamu, maeneo ya biashara, migahawa pamoja na eneo la michezo kwa watoto. Wakazi pia watanufaika na uwepo wa Infinity Hills Mall inayotarajiwa kujengwa, itakayojumuisha maduka ya rejareja, migahawa na vinywaji (F&B), pamoja na ofisi za kisasa ndani ya jengo maalum la biashara.

“Tumeubuni mradi huu kuunganisha makazi, biashara na huduma za mtindo wa maisha ndani ya eneo moja yaliyopangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu,” alisema Bw. Saba.

“Jengo la biashara lenye maduka, migahawa na ofisi litaongeza urahisi kwa wakazi wa eneo hilo na wakati huohuo kuwa kitovu hai cha kiuchumi kwa jamii.”

Mbali na kuwa makazi ya kisasa, Infinity Hills pia inatajwa kuwa fursa madhubuti ya uwekezaji, kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya makazi bora Zanzibar.

 Baadhi ya vivutio vya uwekezaji ni pamoja na eneo lake la kimkakati ndani ya Stone Town, ukaribu na moja ya bustani kubwa za umma kisiwani, ukaribu na bahari, ruhusa ya umiliki kwa wageni pamoja na huduma za usimamizi wa upangishaji baada ya mauzo.

“Infinity Hills inawapa wawekezaji nafasi ya kunufaika na mapato ya upangishaji, ongezeko la thamani ya mitaji kwa muda mrefu na usimamizi wa upangishaji usio na usumbufu,” alisema Bw. Saba.

“Kwa ubora wa hali ya juu katika ukamilishaji wa majengo, huduma bora na eneo la kimkakati, mradi huu unatoa tafsiri ya makazi ya kifahari Zanzibar.”

Baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria, Infinity Developments imesema ujenzi utaanza kulingana na mpango wa utekelezaji wa awamu za mradi huo.

“Timu yetu imefanya kazi kwa shauku na kujituma kugeuza maono haya kuwa uhalisia,” alisema Bw. Saba.

“Nina imani Infinity Hills itazidi matarajio na kuweka alama mpya ya viwango vya makazi Zanzibar.”

Kuhusu Infinity Developments

Infinity Developments ni kampuni inayoongoza Zanzibar katika sekta ya uendelezaji wa majengo, ikiwa na dhamira ya kubadilisha maeneo ya kipekee kuwa uzoefu wa kudumu. Kupitia ubora wa usanifu majengo, uhifadhi wa tamaduni na ubunifu endelevu, kampuni hiyo inatekeleza miradi inayohamasisha, kuwezesha na kudumu vizazi na vizazi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments