Wednesday, February 4, 2026
spot_img
HomeMichezoJeep la Baba Levo lapata ajali Kigoma

Jeep la Baba Levo lapata ajali Kigoma

Gari la Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo, limepata ajali mkoani Kigoma likiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.

Gari hilo ambalo Mbunge huyo alikuwa amewakabidhi wananchi wake kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo harusi, lilipata ajali hiyo katika mazingira ambayo bado hayajawekwa wazi rasmi.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Baba Levo amethibitisha tukio hilo kwa kuchapisha ujumbe na picha zinazoonyesha hali ya gari hilo baada ya ajali, huku akiwaeleza wananchi kuhusu tukio hilo.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu uwepo wa majeruhi au chanzo halisi cha ajali hiyo, huku wadau na wananchi wakitoa pole na salamu za heri kupitia mitandao ya kijamii.

Tutaendelea kuwajuza pindi taarifa zaidi zitakapopatikana.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments