JKT Tanzania yaanza kambi, lengo ubingwa

Kikosi cha JKT Tanzania kinaanza kambi jijini Dar es Salaam leo kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu.

Msemaji Masau Bwire amesema usajili umekamilika kwa asilimia 99 na wamedhamiria kutwaa ubingwa, japo wanatambua ushindani mkubwa unaotarajiwa.

Amesisitiza kuwa hawataishia kuwa wasindikizaji wa Simba na Yanga, bali wanataka kumaliza angalau ndani ya Nne Bora.

JKT tayari imeachana na wachezaji saba, akiwemo Mateo Antony na Ismail Nakapi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *