JKT Tanzania ipo kambini Arusha kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu, ambapo inatarajia kucheza mechi ya kirafiki Ijumaa hii ikisubiri kupatikana mpinzani.

Kocha Ahmad Ally amesema lengo ni kumaliza msimu ujao kwenye nafasi ya juu zaidi ya ya sita waliyoshika msimu uliopita, akiwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono.


