JKU Princess kujipanga kwa CECAFA

JKU Princess ya Zanzibar itaanza kambi Jumatatu kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayofanyika Septemba 4–12 jijini Nairobi.

Timu itapiga kambi Dar es Salaam au Dodoma kwa ushirikiano na Fountain Gate, ili kupata mechi za kirafiki zenye ushindani.

Katibu Shazil Khatibu amesema wataongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi na kuweka historia ya kufuzu ngazi ya CAF.

Bara litawakilishwa na JKT Queens.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *