JKU yapinga usajili wa Nizar na Yanga

Uongozi wa klabu ya JKU ya Zanzibar umesema haujahusika kumuuza mchezaji Abubakar Nizar kwenda Yanga.

Nizar, aliyekuwa kwa mkopo JKU akitokea Azam FC, ametambulishwa na Yanga kama mchezaji wao mpya kuelekea msimu wa 2025/2026.

Katibu wa JKU, Shazil Khatibu, alisema walimrejesha Azam FC baada ya mkataba wa mkopo kumalizika na hawana taarifa zozote kuhusu uhamisho huo. Azam FC tayari imewasilisha malalamiko kwa TFF dhidi ya Yanga kwa madai ya kuvunja taratibu za usajili.

Khatibu alishauri pande zote kukaa pamoja ili kumaliza mvutano huo na kumwezesha mchezaji kuendelea na soka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *