Josiah Karibia kujiunga na Namungo

Namungo FC ipo kwenye hatua za mwisho kumtangaza Kocha wa Prisons, Amani Josiah, kuchukua nafasi ya Juma Mgunda aliyeondoka baada ya kumalizika kwa mkataba.

Josiah aliiokoa Prisons kwenye ‘play off’ dhidi ya Fountain Gate na anasifika kwa kufundisha soka la kisasa.

Namungo imeachana na wachezaji 11 na inatarajia kumtambulisha Josiah mara baada ya makubaliano na Prisons, ambayo imemtangaza Mkenya Zedekiah Otieno kama kocha mpya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *