Klabu ya Junguni United ya Zanzibar imepanga kusajili wachezaji 13 kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu 2025/26, ili kuimarisha kikosi na kuepuka makosa ya msimu uliopita.

Katibu Mkuu, Suleiman Muidani Hassan, amesema wachezaji hao wataimarisha safu ya ushambuliaji, viungo na ulinzi. Usajili utahusisha wachezaji kutoka Zanzibar na Bara.
Amesisitiza kuwa maandalizi ya mapema yatawasaidia wachezaji wapya kuungana vyema na waliobaki. Huu unakuwa msimu wa pili kwa Junguni United kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya kusalia kwa tabu msimu uliopita.