Jussa: Hatutakubali Chama kuvurugwa kwa maslahi binafsi

Zanzibar — Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amesema chama hicho hakitavumilia kuona baadhi ya wanachama wakikivuruga kwa maslahi binafsi ya kutafuta nafasi za Ubunge na Uwakilishi, huku wakipuuza dhamira ya muda mrefu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar.

Jussa amesema chama hicho kilianzishwa kwa misingi ya kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi wa nchi, hususan Zanzibar, na kwamba mwelekeo huo haupaswi kupotoshwa kwa tamaa binafsi za kisiasa.

“Hatupo tayari kuona watu wanakiingiza chama kwenye migogoro kwa sababu ya tamaa ya Ubunge au Uwakilishi, wakati dhamira yetu kubwa ni kushika dola na kuleta mabadiliko ya msingi kwa wananchi wa Zanzibar,” alisema Jussa.

Alisisitiza kuwa ACT-Wazalendo itaendelea kuisimamia ajenda yake ya muda mrefu ya kuwania Urais Zanzibar, kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha ustawi wa Wazanzibari.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *