Kadi nyekundu ya kwanza CHAN yatolewa kwa kiungo wa Madagascar

Mchezaji Andriamirado Aro Hasina wa Madagascar ameandikisha historia ya kuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye fainali za CHAN 2024 zinazoendelea Kenya, Uganda na Tanzania, baada ya kupewa kadi ya pili ya njano dakika ya 37 dhidi ya Mauritania kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Aidha, katika mchezo mwingine wa kundi A, beki wa Angola, Joaquim Balanga, alijifunga mwenyewe dakika za mwisho dhidi ya Morocco, na kuifanya timu yake kupoteza kwa mabao 2-0.

Haya ni matukio ya kwanza ya aina hiyo katika CHAN ya mwaka huu, yakifanana na matukio kama hayo yaliyotokea kwenye CHAN iliyopita nchini Algeria.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *