
MAMLAKA ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA )imeteketeza jumla ya ekari 1,165 za mashamba ya Bangi pamoja na kukamata kilogramu 102 za mbwgi za bangi katikavijiji vya Mafumbo na Lujenge mkoani Morogoro.
Akizungumza Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo (DCEA)Aretas Lyimo baada ya uteketezaji huo alisema mashamba hayo yalikua yamelimwa pembezoni mwa mto Mbakana,Misigiri, na Mgeta katika eneo la akiba la hifadhi Taifa Mikumi.
“kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama tumwfanya operesheni maalum mkoani Morogoro kwa muda wa siku tisa katika vijiji vya Nyarutanga, Lujenge na Mafumbo vilivyopo wilaya za Morogoro vijijini na Kilosa” anafafanua Kamishna Lyimo.
Alisema kuwa,Uharibifu mkubwa wa mazingira umefanyika katika eneo hilo ambapo miti imekatwa ili kupata eneo la kulima bangi na hivyo kuharibu uoto wa asili “Kijiji cha Nyarutanga watu 6 wakiwa na kilogramu 342 za bangi wamekamatwa na watafikishwa mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika”.


Pia uharibifu uliofanyika katika eneo la akiba la Mikumi unaharibu ikolojia ya eneo hilo na kufanya uharibifu mkubwa wa uoto wa asili na ikizingatiwa mito hiyo inatiririsha maji katika bwawa la Mwalimu Nyerere linalotegemewa kwa uzalishaji wa umeme hapa nchini.
Katika hatua nyingine amwqapongwza vijana walioonyesha uzakwndo katika kushiriki uteketezaji qa mashamba hayo ya kilimo haramu Cha mmea aina ya Bangi “Mamlaka Tumshukuru pia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwesesha operesheni mbalimbali kuendelea kufanyika hapa nchini.
Aidha aliwleza ,Mamlaka hiyo imejipanga vyema kuendelea kutekeleza dhamira ya serikali ya awamu ya sita Kwa kuhakikisha wanalinda afya za wananchi kwa kuhakikisha kuwa Dawa za kulevya zinadhibitiwa hapa nchini.
“Tunahakikiaha tunadhibiti kilimo Cha bangi, mirungi pamoja na kudhibiti kemikali bashirifu na matumizi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya ambaO baadha ya watu hutumia kama mbadala wa dawa za kulevya” alisema Kamishna Lyimo.



Alitoa Wito kwa wakazi wa Mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo kupifa vita kilimo haramu Cha mmea aina ya Bangi huku akiwaeleza kuwa Msimamo wa mamlaka hiyo ni kutowafumbia macho wale wote qanaojishughulisha na biashara ya Dawa za kulevya nchini.
Saidi Mijinga mkazi wa Kisaki alisema eneo lililotumika kulima bangi ni kubwa sana, endapo lingetumika kulima mazao mengine wananchi wangenufaika kwani mazao hayo hulimwa bila kificho na kuuzwa kwa uwazi jambo ambalo lingewaletea faida ya chakula na kipato.
“Ninawashauri wanaolima bangi waache hii tabia walime mazao mengine ili tufaidike wote kwa sababu kuna kunde, mahindi, choroko, maharage na mbaazi yote haya yanakubali. Hili eneo ni kubwa sana linaweza likatulisha sisi kijiji na kuifanya njaa isiwe gumzo. Kwani kuna muda unafika vyakula hakuna zipo bangi tu, Sisi hatuwezi kula bangi†amesema.
Naye Joseph Juma Kibaya mkazi wa Nyarutanga amewaomba wananchi waendelee kuwafichua wauzaji na wafanyabiasha wa bangi kwani inamadhara makubwa kwa vijana na jamii kwa ujumla, na kuomba raia waungane na kuwa kitu kimoja kupinga bangi ili kuepuka athari zake kwa vijana na vizazi vya baadaye.