Dar es Salaam, Agosti 6, 2025 – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mstaafu, Jamal Rwambow, amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo.

Rwambow alipokelewa na Kiongozi wa Chama hicho, Dorothy Semu, katika hafla maalum iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Magomeni, mkoani Dar es Salaam.
Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, wanachama na wafuasi waliokuja kushuhudia hatua hiyo muhimu ya mwanachama mpya kujiunga na harakati za kisiasa ndani ya ACT Wazalendo.




