Kampeni ya kuchangia Damu yazinduliwa Bunju, Dar


Kampeni ya kuchangia damu kupitia vyuo vya afya vya kati na vikuu imezinduliwa jijini Dar es Salaam, ambapo wakazi wa Bunju, Boko na Tegeta wameungana na wanafunzi wa vyuo hivyo kuchangia damu. Zaidi ya chupa 200 za damu zimekusanywa katika zoezi hilo lililofanyika Bunju, Wilaya ya Kinondoni.

Frederick Mbinga na Neema Gozibart, miongoni mwa wachangiaji damu, walisema wanachangia damu kwa sababu wanatambua umuhimu wake katika kuokoa maisha ya wagonjwa.

Afisa Uhamasishaji wa Damu Salama kutoka Wizara ya Afya, Evelyn Dielly, alisema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na umeonyesha mafanikio ya kampeni hiyo. Dkt. Hilda Tutuba kutoka MUHAS alieleza kuwa damu salama ni muhimu kwa wagonjwa wa sikoseli na mahitaji mengine ya kiafya.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Keneth Woiso, aliipongeza kampeni hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama nchini.


Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *