Kaseke, Mpole waaga rasmi Pamba Jiji


Klabu ya Pamba Jiji imetangaza kuachana na wachezaji wanne, akiwemo Deus Kaseke aliyejiunga dirisha dogo na kusaidia timu kusalia Ligi Kuu. Hii inafuatia kuachwa kwa mshambuliaji George Mpole, aliyekuwa mfungaji bora wa msimu wa 2021/22.

Wengine walioachwa ni Mwaita Gereza, Paul Kumtewe na Ally Ramadhani ‘Oviedo’. Hii ni baada ya kutangazwa kwa kocha mpya, Francis Baraza, akichukua nafasi ya Fred Minziro aliyemaliza mkataba.

Hadi sasa, Pamba Jiji imeachana na jumla ya wachezaji tisa, akiwemo Mpole aliyefunga mabao 17 akiwa na Geita Gold, akimpiku Fiston Mayele wa Yanga. Wengine walioachwa awali ni Lazaro Mlingwa, Modou Camara, Ibrahim Ishaka, Cherif Ibrahim na Abalkassim Suleiman.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *