Monday, March 9, 2026
spot_img
HomeBiasharaKCB yashiriki Mkutano wa Wakuu EAC Arusha

KCB yashiriki Mkutano wa Wakuu EAC Arusha

Benki ya KCB Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Cosmas Kimario, imeshiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jijini Arusha.

Ushiriki wa benki hiyo umejikita katika kuchangia majadiliano yanayolenga kuimarisha maendeleo ya fedha za kidijitali, kukuza masoko ya mitaji pamoja na kurahisisha biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika mkutano huo, uzinduzi wa mfumo wa EAC Customs Bond umetajwa kuwa hatua muhimu itakayosaidia kuimarisha biashara ya mipakani na kurahisisha shughuli za wafanyabiashara wanaofanya biashara ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Hatua hiyo pia inatarajiwa kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa bidhaa na kuchochea ukuaji wa biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments