Kelvin Nashon atemwa kwa mkopo, ajiunga na Pamba Jiji

Kiungo mkabaji Kelvin Nashon amejiunga na Pamba Jiji kwa mkopo akitokea Singida Black Stars.

Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza, amesema wamefanya hivyo ili kumpa nafasi zaidi ya kucheza, kutokana na ushindani mkubwa unaotarajiwa kwenye kikosi msimu ujao.

Nashon bado ana mkataba na Singida, na uamuzi huo umetokana na sababu za kiufundi, ili kukuza kiwango chake kwa kupata mechi nyingi zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *