Kesi ya wenyewe kwa wenyewe, CHADEMA yafungiwa siku 14

Bundi ameendelea kutua kwenye viunga vya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya Mahakama Kuu kukifungia chama hicho kufanya shughuli zake za kisiasa kwa siku 14.

Kesi hiyo namba 8323 ya mwaka 2025 imefunguliwa na mwanachama wake Said Issa Mohamedi na wenzake wawili, ikisikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga.

Uamuzi huo umekuja kutonesha kidonda cha Chadema, baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kutowatambua viongozi wake kadhaa, akiwemo John Mnyika, Katibu Mkuu wake, akisema kuwa upatikanaji wa viongozi hao ulikuwa na dosari.

Kwa kufungiwa kwa Chadema, watalazimika kusitisha ziara zao wanazofanya mikoani wakinadi chama chao katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *