Saturday, November 1, 2025
spot_img
HomeElimuKibonde aahidi kuweka kipaumbele sekta ya elimu akiwa rais 

Kibonde aahidi kuweka kipaumbele sekta ya elimu akiwa rais 

Musoma, Mara – Mgombea Urais kupitia Chama cha Makini, Ndugu Coaster Kibonde, ameahidi kuipa sekta ya elimu kipaumbele cha kwanza endapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Saa Nane, Wilaya ya Musoma, Kibonde alisema serikali yake itahakikisha walimu wanaboreshewa mazingira ya kufanyia kazi na kupewa heshima wanayostahili, hasa wale wanaofundisha katika shule za vijijini ambako bado kuna changamoto kubwa ya upungufu wa walimu.

“Nimepita shule nyingi za vijijini na kubaini walimu wachache sana wanapendelea kufundisha huko kutokana na mazingira magumu yaliyopo. Nikiingia madarakani, serikali yangu itahakikisha tatizo hilo linaisha,” alisema Kibonde.

Aliongeza kuwa walimu ni uti wa mgongo wa taifa, lakini kwa muda mrefu wamesahaulika licha ya mchango wao mkubwa katika maendeleo ya nchi.

“Bila juhudi za walimu, mimi mwenyewe nisingefika hatua ya kugombea urais. Serikali ya Chama cha Makini itarejesha heshima yao,” alisisitiza Kibonde.

Kibonde alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka wananchi wa Mara na Watanzania kwa ujumla kuunga mkono sera za Chama cha Makini, akiahidi kujenga taifa lenye elimu bora, usawa, na motisha kwa walimu wote nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments