Rais mstaafu wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete amemhakikishia Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa wananchi watawachagua wagombea ubunge na udiwani wa CCM, bila kuchanganya.
Dkt Kikwete ameyasema hayo leo, Jumapili Septemba 28, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais, uliofanyika wilayani Kibaha katika Mkoa wa Pwani.Amesema anatambua umuhimu wa kumwezesha afanye kazi kwa ufanisi kwa kumpatia wabunge na madiwani wa CCM.
“Tunakuhakikishia kama bunge linalomalizika sasa, wabunge wote wa CCM na litakalokuja kutoka Pwani wabunge wote wa CCM na naamini nchi nzima itakuwa hivyo.
“Hatuko tayari mheshimiwa Rais na mgombea wetu, kuchanganya pumba na mchele. Tunayajua madhara yake na hatutathubutu kufanya hivyo,” amesema.




