Kocha wa Kenya asifu ushindi dhidi ya DR Congo

Kocha wa Harambee Stars, Benni McCarthy, amesifu nidhamu na ujasiri wa wachezaji wake baada ya Kenya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya DR Congo kwenye mechi ya Kundi A ya CHAN, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.

McCarthy amesema wachezaji wake wengi walikuwa wakicheza mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza na walionyesha ujasiri mkubwa licha ya hofu ya awali. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Austin Odhiambo dakika ya 45+2.

DR Congo ni mabingwa mara mbili wa CHAN, walitwaa taji hilo mwaka 2009 na 2016. Kenya itacheza mechi yake ijayo dhidi ya Angola Alhamisi ijayo, kwenye uwanja huo huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *