Yanga SC imemtangaza Manu Rodriguez, aliyewahi kufundisha Olympic Lyon na timu za taifa za Venezuela na Costa Rica, kuwa kocha msaidizi wa Romain Folz.

Pia imemleta kocha wa utimamu wa mwili Tshephang Mokaila (Afrika Kusini/Botswana), aliyekuwa Al Ahli Tripoli ya Libya.
Rodriguez anachukua nafasi ya Abdulhamid Moalin huku Mokaila akibeba mikoba ya Taibi Lagrouni.
Yanga pia imeongeza mkataba wa miaka miwili kwa mshambuliaji wa DR Congo Maxi Nzengeli, aliyepachika mabao 6 na kutoa asisti 10 msimu uliopita.