Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeBiasharaKongani ya TPC kuleta ajira 1,800 na nishati safi Moshi

Kongani ya TPC kuleta ajira 1,800 na nishati safi Moshi

Ujenzi wa kongani ya viwanda vya TPC vinavyolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo hai, kuzalisha umeme wa nishati jadidifu, hewa ukaa na nishati ya Ethanol kwa ajili ya kupikia, unatarajiwa kufungua fursa mpya za kiuchumi, kutoa ajira 1,800 kwa Watanzania na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kongani hiyo ambayo inatumia masalia ya mazao ya miwa (molasesi), inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 52, sawa na Sh bilioni 130. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Novemba 18, 2025) na Afisa Mtendaji wa Utawala wa TPC, Jaffari Ally, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, anatarajiwa kesho (Novemba 19) kuweka jiwe la msingi katika kongani hiyo inayojengwa katika Kata ya Arusha Chini, Wilaya ya Moshi.

Kongani hiyo inatarajiwa kuzalisha lita milioni 16.3 za Extra Neutral Alcohol (Ethanol – ENA), pamoja na lita 400,000 za Technical Alcohol kwa ajili ya matumizi ya majiko poa majumbani. Pia itazalisha mbolea aina ya Potassium takribani tani 8,000 itakayopatikana baada ya uchakataji wa molasesi wakati wa uzalishaji wa Ethanol.

Aidha, kongani hiyo itazalisha lita 400,000 za hewa ukaa (carbon dioxide) kwa matumizi ya viwandani, pamoja na mitambo ya kuzalisha umeme megawati 6 ambao utaunganishwa na kuuzwa kwa TANESCO.

“Miradi hii ikikamilika Disemba 2026, tutaboresha ajira, uwezo wetu wa kulipa na kukusanya kodi, na kuboresha mazingira kwa kusaidia juhudi za serikali kuwa na nishati safi na salama,” alisema Ally.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments