Timu ya Netiboli ya KVZ imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chake kuelekea mashindano ya kimataifa, baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Netiboli Zanzibar kwa mara ya tano mfululizo, na pia kushinda Kombe la Muungano mwaka huu.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Abduljalili Mohmed, amesema lengo kubwa ni kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki. Amesema timu hiyo imekuwa ikitawala mashindano ya ndani, hivyo sasa wanataka kuweka historia kimataifa.
KVZ pia inatarajia kusajili wachezaji wapya na kuwapa mikataba wale watakaosaidia kufikia malengo hayo ya kimataifa.