Saturday, March 21, 2026
spot_img
HomeMichezoKwanini Stars ilishindwa kuvuka makundi licha ya ubora wa wachezaji wake?

Kwanini Stars ilishindwa kuvuka makundi licha ya ubora wa wachezaji wake?

Mataifa mengi ya Afrika yameendelea kuonyesha kuwa mafanikio ya timu za taifa hayategemei wachezaji wanaocheza nje pekee, bali uimara wa ligi za ndani na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo.

Mfano hai ni Misri, ambapo takribani asilimia 75 ya kikosi cha timu yao ya taifa kinaundwa na wachezaji wanaocheza ndani ya ligi ya nchini humo. Vivyo hivyo kwa Afrika Kusini, ambako karibu asilimia 80 ya wachezaji wa Bafana Bafana wanatoka kwenye Ligi Kuu ya PSL.

Sudani ni mfano mwingine wa kuvutia zaidi. Takribani asilimia 90 ya wachezaji wa timu yao ya taifa wanatoka kwenye ligi ya ndani, licha ya ukweli kwamba tangu mwaka 2023 hawakuwa na ligi inayoendelea.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba katika michuano ya AFCON, zaidi ya wachezaji watatu walioteuliwa kwenye kikosi cha taifa hawakuwa wanacheza kwenye klabu yoyote, lakini bado waliweza kufika hatua ya 16 bora.

Nikirejea hoja yangu ya leo, ni wazi kuwa wachezaji wetu wa ndani kama Job, Nangu, Mwalimu, Feisal na Bacca wanacheza kwenye mashindano makubwa ya kimataifa, wakikutana na wachezaji wa kiwango cha juu kama Teboho, Zizo na Abdelrahiman katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Swali la msingi linabaki: kwa mazingira haya yote, ilikuwaje Taifa Stars ishindwe hata kushindana kwa kiwango cha kuvuka hatua ya makundi?

Ukweli ni kwamba Taifa Stars ilikosa uongozi sahihi katika benchi la ufundi. Kulikosekana kocha mwenye uwezo wa kuisoma timu pinzani na kuja na mpango kazi madhubuti, kocha asiyeangalia majina ya wachezaji bali uwezo na mchango wao uwanjani, pamoja na kocha anayeweza kutumia kikamilifu wachezaji waliopo kuunda kikosi cha ushindani.

Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania haiwezi kuwa Senegal hata kama zingepita miaka 100,000, wala Taifa Stars haiwezi kufikia hadhi ya Algeria hata kama dunia ingezunguka mara 20,000. Hata hivyo, hiyo haimaanishi kuwa hatuwezi kuijenga Taifa Stars imara, yenye ushindani na inayocheza mpira wa kisasa, kama ambavyo mataifa mengine ya Afrika yalivyofanya.

Mwanzo mzuri umeonekana chini ya kocha Gamondi katika michuano ya AFCON ya kushitukiza, ambapo tumeshuhudia Taifa Stars ikicheza mpira wa kuvutia, ikipeleka ushindani uwanjani na kuonyesha mwanga wa matumaini kwa siku zijazo. Nina imani kubwa kuwa Gamondi ana uwezo wa kuisuka upya Taifa Stars na kuijenga timu bora.

Hii ndiyo Taifa Stars ambayo mashabiki walikuwa wanaiota.

✍️ Kalamu ya Ushahidi
@cheyolutenganotz

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments