Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema kuwa upande wa utetezi unasistiza kuendelea kwa matangazo ya moja kwa moja (live streaming) ya mwenendo wa kesi ili umma na dunia kwa ujumla waone kinachoendelea mahakamani.

“Mnachoruhusiwa kuficha ni kile alichokisema Jaji na si vingine. Wanataka kusogeza bahasha, kuingiza mambo ambayo hayapo kwenye oda ya Jaji. Aliyosema Jaji yasiwe kwenye publication, ni sawa. Mengine yote ruksa,” amesema Lissu.
Ameongeza kuwa kauli ya upande wa mashtaka inayohoji sababu ya kuendelea na live streaming haina mashiko, akisisitiza umuhimu wa uwazi wa mwenendo wa kesi.
“Wakili wa Serikali amesema haoni sababu ya kung’ang’ania Live Streaming iendelee. Sasa namjibu, tunang’ang’ania Live Streaming ili dunia na umma wote uone kinachoendelea. Hii ndiyo sheria niliyofundishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilipokuwa kijana,” amesema Lissu.