López: Mauritania ina matumaini CHAN

Kocha wa Mauritania, Garay Ortiz López, amesema matumaini ya timu yake yamefufuka baada ya kupata ushindi wa kwanza kwenye CHAN dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Kundi B uliwapa Mauritania pointi tatu na nafasi ya pili, ukiwaweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.

López alisema mchezo ulikuwa mgumu lakini wachezaji wake walionesha kiwango kizuri na walitengeneza nafasi nne za kufunga, wakafanikiwa kupata ushindi muhimu katika kampeni zao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *