Takwimu zinaonesha mabao 56 yamefungwa katika michezo 35 ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu — wastani wa bao 1.6 kwa kila mchezo.
Kati ya hayo, 46 yamefungwa ndani ya boksi na 10 nje ya eneo la hatari. Wachezaji 44 wamefunga, huku nyota wa JKT Tanzania, Salehe Karabaka na Paul Peter, wakiongoza kwa mabao matatu kila mmoja.
Michezo 23 imetoa washindi huku 12 ikimalizika kwa sare. Mechi nyingi zenye ushindi (17) zimechezwa nyumbani.
Ligi itaendelea keshokutwa kwa michezo mikubwa: Pamba Jiji vs Singida Black Stars kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, na Simba SC vs JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.




