Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Pete Tanzania (CHANETA) imepanga kuendesha Ligi Kuu ya Netiboli itakayoanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkuu, Kassim Ahmad, alisema lengo ni kufufua mchezo huo na kuufikisha viwango vya kimataifa, wakipanga pia kwenda mikoani kukutana na maskauti ili kuunda Timu ya Taifa imara.
Kwa sasa, Samia Netball Cup inaendelea viwanja vya Garden, Magomeni, ambapo JKT na Magereza zinaongoza kwa pointi sita kila moja, zikifuatiwa na KIUT yenye pointi nne.
Ofisa Habari wa taasisi hiyo, Lilian Mahalu, alisema mwamko umeongezeka na timu nyingi zimeomba kushiriki. Mwenyekiti wa CHANEDA, Pili Mogella, alisema mashindano hayo yameibua vipaji vipya na viwango bora vya wachezaji chipukizi.