Masala Princess kuandaa bonanza la michezo Dar


Klabu ya Masala Princess imeandaa bonanza la michezo litakalofanyika Agosti 14-17 kwenye viwanja vya JMK, Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Esther Mpanda, amesema lengo ni kuibua vipaji na kuhamasisha ushiriki wa michezo kwa vijana wa jinsia zote, wakiwemo watu wenye ulemavu chini ya umri wa miaka 20 na 13.

Timu nane za wanawake zimesajiliwa, zikiwemo Ilala Queens, Mbagala Queens, Masala Princess, Kinondoni Queens, Wisdom Queens, Sayari Queens, The Eleven Queens na Young Stars.
Washindi watapewa makombe na medali, huku timu ya Masala ikiendelea na mazoezi kila siku.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *